Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameiagiza bodi
ya Shirika la Nyumba la Taifa Nyumba (NHC) kuacha kuanzisha miradi mipya
ya ujenzi hadi kukamilishwa kwa miradi iliyokwishaanza.
Akizungumza
na wajumbe wa bodi hiyo Dar es Salaam jana, Lukuvi alisema hakuna haja
ya kuanzisha miradi mipya wakati iliyopo haijakamilika.
“Nadhani
miradi iliyopo mnaijua na tarehe za kukamilika ujenzi wake wote
tunafahamu, hivyo nitoe agizo kuanzia leo hakuna kuanza kwa mradi mpya
wowote mpaka imalizwe iliyokwishaanza,” alisema.
Lukuvi
pia aliiagiza bodi hiyo kutopandisha kodi za nyumba zake bila ridhaa
yake huku akisisitiza gharama zipangwe kwa kuzingatia uwezo wa wananchi.
“Hamuwezi
kusema nyumba ya gharama nafuu wakati ina vyumba viwili na inauzwa kwa
Sh52 milioni, hainiingii akilini na wala Mtanzania wa kawaida hawezi
kuona unafuu wowote hapo,” alisema Lukuvi.
0 comments:
Post a Comment