WAZIRI
Mkuu, Kassim Majaliwa ameitaka wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera kudhibiti
usafirishaji haramu wa madini ya bati, akieleza kuwa yuko mwanamke
ambaye si rais wa Tanzania anayesafirisha kinyume cha utaratibu.
Alitaka
kujua hatua zilizochukuliwa kudhibiti hali hiyo na kumhoji Mkuu wa
Wilaya, Benedict Lenga endapo anafahamu watu wanaosindikiza wezi hao wa
madini.
“Madini ni tija, lazima tujue yanasafirishwa kwa kigezo kipi.Tunajua wakati mwingine tunasindikiza watu wanaoiba madini yetu,” alisema Majaliwa na kuhoji endapo Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) ndiye anayesindikiza. Hata hivyo, alijibiwa kuwa hahusiki.
Aidha,
alimtaka Lenga na watu wake waimarishe ulinzi ili biashara hiyo ya
madini idhibitiwe. Majaliwa alikuwa akizungumza baada ya kupokea taarifa
ya mkoa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa, John Mongella, alipowasili hapa jana
kuanza ziara ya siku nne.
0 comments:
Post a Comment