Madiwani
watatu wa Chadema na mfuasi mmoja wa chama hicho wamefikishwa katika
Mahakama ya Wilaya ya Rombo kwa makosa ya kufanya uchochezi.
Madiwani
hao, Nicolaus Kimario (Kirio), Anasia Kimario (Viti Maalumu), Daud
Tarimo (Leto ) na mfuasi wa Chadema, Rogath Kanje walikana mashtaka
hayo.
Mwendesha
mashtaka, Bernard Machivya alieleza mahakama kuwa washtakiwa walitenda
kosa hilo Agosti 25, wakiwa nyumbani kwa mmoja wa washtakiwa Nicolaus
Kimario.
Aliieleza
Mahakama kuwa washtakiwa wote wanne walitenda kosa hilo kwa pamoja
wakifanya vikao vya kuhamasisha wananchi wajitokeze kwenye maandamano ya
Ukuta Septemba Mosi.
Hakimu
Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Rombo, Naomi Mwerinde aliahirisha
kesi hiyo hadi Septemba 5 na watuhumiwa wote wataendelea kukaa rumande.
0 comments:
Post a Comment