Tume
ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imesikitishwa na matamshi
ya Mhe. Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam yanayokiuka misingi
ya utawala bora aliyoyatoa tarehe 25 Agosti, 2016 wakati wa kuaga miili
ya askari Polisi watatu waliouawa Mbande, Mkoani Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Bahame Tom Nyanduga, leo (Agosti 26,
2016) Mhe. Makonda ametumiwa barua ya wito inayomtaka afike makao makuu
ya Tume mtaa wa Luthuli, tarehe 30 Agosti, 2016 ili kujadili kile Tume
ilichokiona kuwa ni kejeli kwa Tume pamoja na jumuiya yote ya watetezi
wa haki za binadamu.
Aidha,
Tume imeona kuwa maagizo aliyoyatoa Mkuu huyo wa Mkoa kwa Jeshi la
Polisi hayana msingi wa kisheria na hayako ndani ya mamlaka ya Mkuu wa
Mkoa.
Kwa
mujibu wa Kifungu cha 6(1)(f) na (i) pia Kifungu cha 27(1) na (2) (a)
vya Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Sura Na. 391 ya
Sheria za Tanzania 2002, THBUB ina mamlaka ya kuchunguza mwenendo wa mtu
au taasisi yoyote kuhusiana na utendaji wa kazi zake zinapokiuka mipaka
ya madaraka yake, ili kuchukua hatua za kurekebisha ukiukwaji huo.
Imetolewa na:
(SIGNED)
Idara ya Elimu kwa Umma na Mafunzo
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
Agosti 26, 2016
0 comments:
Post a Comment