Ilikuwa ni kama filamu ya
askari na maadui wakati askari wa Jeshi la Polisi walipopambana na watu
wanaosadikiwa kuwa ni majambazi kwenye nyumba iliyo eneo la Vikindu
wilayani Mkuranga.
Taarifa ambazo zimepatikana kutoka kwa watu waliokuwa karibu na operesheni hiyo na ambazo hazijathibitishwa na mamlaka rasmi, zinasema kamishna wa Kitengo cha Kuzuia Ujambazi, ASP Thomas Njuki aliuawa kwa kupigwa risasi kichwani.
Taarifa hizo zilisema
kuwa jambazi mmoja aliuawa ingawa idadi ya waliokamatwa haikufahamika
mara moja kutokana na mashuhuda kutoa takwimu tofauti.
Kamanda wa Polisi
wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema ataongea na
waandishi wa habari leo saa 4:00 asubuhi kuzungumzia tukio hilo.
Tukio
hilo limetokea siku chache baada ya askari wanne wa Jeshi la Polisi
kuuawa wakati wakibadilishana lindo kwenye tawi la benki ya CRDB
lililoko Mbande jijini Dar es Salaam.
Watu hao, waliofika wakiwa
wamepanda pikipiki, walipora silaha na kutoweka nazo. Katika tukio la
jana, askari wa Jeshi la Polisi walikuwa na nia ya kuwakamata watu
waliowashuku kuwa ni majambazi.
Kwa mujibu wa watu wanaoishi karibu na
nyumba hiyo, mpambano kati ya polisi na majambazi hao ulianza saa 7:30
usiku baada ya polisi kuvamia nyumba walimopanga majambazi hayo.
Tukio lilivyotokea
Chanzo kimoja cha habari kimeeleza kuwa baada ya polisi kufuatilia nyendo za wakazi wa nyumba hiyo walianza upelelezi na kubaini kuwa huenda wanahusika na matukio kadhaa ya uhalifu, likiwamo la uvamizi wa kituo cha polisi cha Stakishari na lile la tawi la CRDB Mbande mkoani Pwani.

Mpashaji huyo alisema kuwa jana saa
saba usiku, polisi walifika kwenye nyumba hiyo iliyo Mtaa wa Vikindu
Mashariki ambayo ina maduka upande wa mbele, ikipakana na nyumbani
nyingine mbili pembeni na nyuma zikiwa umbali usiozidi hatua nne.
Habari
hizo zinasema askari hao kwanza walimtuma mwenyekiti wa serikali ya
mtaa kwenda kuwasihi wafungue mlango na walipokataa ndipo walipoenda
kugonga, wakiwaamrisha watu hao wafungue mlango.
“Baada ya kuona hawatii
amri ya kufungua mlango, polisi waliamua kuvunja vitasa kwa kutumia
bastola, ndipo risasi zikaanza kurushwa,” alisema mpashaji habari huyo.
“Kwa kuwa mkuu alikuwa mbele, wahalifu walimpiga risasi kichwani na alikufa palepale.”
Mtu huyo alisema kuwa baada ya Kamishna Njuki kufariki, askari wengine walirudi
nyuma kujihami zaidi.
Baada ya hapo polisi waliendelea kupiga risasi kuelekea maeneo mbalimbali ya nyumba hiyo na wahalifu hao kujibu mashambulizi.
“Kila chumba ambacho polisi walikuwa wakijaribu kurusha risasi, zilijibiwa. Inaelekea kila chumba kilikuwa na mtu mwenye silaha,” alisema shuhuda mwingine wa tukio hilo.
Habari kutoka kwa majirani zinasema hadi saa 2:45 asubuhi, milio ya risasi iliendelea kurindima katika eneo hilo.

Baadaye polisi waliomba kuongezewa nguvu na
Jeshi la Wananchi (JWTZ) ambao walifika na kuendeleza mapambano hayo.
Mtoto ataja alipojificha baba
Wakati mapambano yakiendelea, sauti za watoto waliokuwa wakilia zilisikika na ndipo askari wa JWTZ waliamuru watu hao wawatoe nje.
Mtoto ataja alipojificha baba
Wakati mapambano yakiendelea, sauti za watoto waliokuwa wakilia zilisikika na ndipo askari wa JWTZ waliamuru watu hao wawatoe nje.
“Watoto walipotoka nje, polisi waliwauliza baba yupo
wapi, mtoto mmoja akajibu yupo darini,” alisema
Baada ya polisi kusikia hivyo, walielekeza mashambulizi yao darini na kufanikiwa kumjeruhi mtu aliyejificha darini ambaye alishuka.
Wakati polisi wakishinikiza atoke ndani ili kujisalimisha, mtu huyo alijipiga risasi mara baada ya kutoka na kufariki dunia.

Wakazi Vikindu wahaha!
Kutokana na tukio hilo, taharuki ilitanda kwa wakazi wa Vikindu na biashara zote zilifungwa eneo hilo huku wananchi wakiwa na chupa za maji kutokana na mabomu ya machozi yaliyokuwa yakipigwa kila mara.

Wakazi wa eneo ambalo lipo
karibu na maegesho ya magari ya Farid Seif, hawakuruhusiwa kutoka ndani
na waliofanikiwa kutoka usiku hawakuingia hadi jana saa 7.00 mchana
wakati hali ilipotulia.
Kutokana na majibizano ya risasi, watu
wanaofanya kazi jijini Dar es Salaam ambao wanaishi vijiji vya Melela,
Vianzi, Pemba Mnazi na Mfuru hawakwenda kazini kutokana na barabara
inayotoka Vikindu kufungwa hadi saa 7.00 mchana.
0 comments:
Post a Comment