Afisa wa ngazi ya juu wa shirika la Umoja wa Mataifa la huuma kwa
wakimbizi, Filippo Grandi, amewatolea wito viongozi wa Sudan Kusini
kumaliza mateso ya watu wao.
Bw Grandi alikua akizungumza na
waandishi wa habari baada ya kukutana na wakimbizi Kutoka Sudan
Kusini wanaoishi kambini magharibi mwa Uganda.
Mashirika ya
Umoja wa Mataifa yanakadiria kuwa zaidi ya watu 80,000 wamewasili
nchini Uganda tangu kuibuka kwa mapigano ya hivi karibuni nchini humo.
Alisema: " Viongozi wa taifa lile changa wanapaswa kuwajibika."
Vikosi
vya wanajeshi watiifu wa viongozi wanaohasimiana kisiasa walikabiliana
kisiasa katika mji mkuu, Juba, mwezi uliopita, suala linalozorotesha
mchakato wa amani uliolenga kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini
humo.
Chanzo: BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment