Serikali
imetangaza rasmi kugundulika kwa futi za ujazo wa Gesi Tirioni 2.17
katika Bonde la Ruvu mkoani Pwani, katika eneo lijulikanalo kama Mamba
Kofi One ikiwa ni moja ugunduzi ulifanywa na Kampuni ya Dodsal
ikishirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
Akitoa tamko hilo mbele ya vyombo vya habari ofisini kwake Dar es Salaam jana asubuhi,
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alisema kuwa
hadi kufikia Machi mwaka huu jumla ya gesi yote iliyogunduliwa nchini ni
trioni 57.23.
"TPDC
imerekebisha muundo wake tunataka iwe inajishughulisha na utafutaji wa
gesi ya mafuta hivyo kufuatana na sheria ya petroli ya mwaka jana kazi
zote zitasimamiwa na TPDC na haitaendelea kusimamia makampuni mengine
badala yake tuameazisha wakala wakusimamia kazi ," alisema Muhongo.
Akitolea
ufafanuzi kuhusiana na kugundulika kwa gesi hiyo asilia iliyopo nchi
kavu imefikia futi za ujazo tirioni 10.17, na baharini katika kina kirefu cha futi za ujazo ni 47.08.
Waziri
Muhongo alisema ufumbuzi huo umefanywa na Shirika la Maendeleo ya
Petroli Tanzania (TPDC) kwa kushirikiana na Kampuni ya Haydrocarbons and
Power Limited (DODSAL) hivyo wakiendelea na utafiti wataweza kuvuka
hata futi 10 kama walivyo dai.
Alisema
kuwa takribani futi za ujazo elfu moja zina uwezo wakuzalisha jumla ya
megawati za umeme zipatazo 5000 wakati huo bado wanaendelea na utafiti
wa gesi katika maeneo ya kusini mwa Tanzania ambapo kumegundulika kuwa
na gesi nyingi .
"Nilazima
taifa letu liwe na umeme mwingi, na umeme wa kutosha kwani tukifanya
hivyo tunaweza kufikia kwenye bigawati kama nchi za kusini walivyoweza
kupata umeme mwingi," alisema Muhongo.
Akijibu
maswali kuhusiana na kunufaika kwa wananchi na gesi hiyo alisema
tayari wameaza kunufaika kwani kabla ya awamu ya tano ya Rais Dk. Jonh
Magufuli, jumla ya megawati 700 hadi 800 ndizo zilikuwa zikitumika
katika matumizi ya umeme ambapo katika kipindi cha awamu ya tano jumla
megawati 1000 zinaendelea kutumika.
"Ifahamike
kuwa faida ya gesi kwa wananchi ni ya siku nyingi kwani viwanda
takribani 37 vimekuwa vikitumika kwa matumizi ya gesi kikiwemo kiwanda
cha Saruji " alisema.
Awali
kabla ya uzinduzi huo Meneja Utafiti wa Shirika la Maendeleo ya Mafuta
na Gesi (TPDC), Venosa Ngowi alisema wanatarajia kumpatia ripoti ya
mapendekezo ya juu ya gharama za uuzaji wa gesi nchini ifikapo Aprili,20
mwaka huu.
Ngowi
alisema zoezi linalofanyika ni mazungumzo ya wawekezaji na watalamu wa
nchi husika kuweza kufanya uhakiki wa gharama wa bei za gesi nchini.
Alisema moja ya changamoto wanazokutanazo ni kuwepo kwa gharama nyingi zinazo muhusu mwekezaji.
0 comments:
Post a Comment